Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 12

Yohana 12:34-46

Help us?
Click on verse(s) to share them!
34Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
35Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.
36Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga.” Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
37Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.
38Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”
39Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:
40“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
41Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
42Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
43Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu
44Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.
45Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.
46Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.

Read Yohana 12Yohana 12
Compare Yohana 12:34-46Yohana 12:34-46