Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 12:34-46 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 12:34-46 in Biblia Takatifu

34 Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
35 Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.
36 Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga.” Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
37 Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.
38 Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”
39 Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:
40 “Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
41 Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
42 Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
43 Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu
44 Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.
45 Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.
46 Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.
Yohana 12 in Biblia Takatifu

Yohana 12:34-46 in Biblia ya Kiswahili

34 Mkutano wakamjibu, “Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, 'Mwana Adamu lazima ainuliwe juu'? Huyu Mwana wa Mtu ni nani?”
35 Basi Yesu akawaambia, “Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako.
36 Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.
37 Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini
38 ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: “Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
39 Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,
40 “Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya.”
41 Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.
42 Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakatengwa na sinagogi.
43 Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
44 Yesu akapaza sauti na kusema, “Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi,
45 naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma.
46 Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
Yohana 12 in Biblia ya Kiswahili