Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 17

Luka 17:11-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya.
12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali
13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.”
14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika.
15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu.
16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.
17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?
18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?”
19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”
20Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana.
21Wala watu hawatasema, 'Angalia hapa!' au, 'Angalia kule!' kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona.
23Watawaambia, 'Angalia, kule! Angalia, hapa!' Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata,
24kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake.
25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.

Read Luka 17Luka 17
Compare Luka 17:11-25Luka 17:11-25