18Mungu ambaye humwambia mfalme, 'Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?
19Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
20Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
21Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
22Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
23Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
24Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
25Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
26Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
27kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
28Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
29Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
30ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
31Fikiria mtu akimwambia Mungu, 'Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
32nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
33Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
34Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,