1Hakika kuna machimbo ya fedha, wanaposafisha dhahabu.
2Chuma uchimbwa; shaba uyeyushwa kutoka katika jiwe.
3Mtu anaondoa giza na kutafuta, katika mpaka wa mbali, mawe hayaonekani na giza totoro.
4Huchimba shimo mbali na makazi ya watu, mahali pasipopitwa na mtu. Huning'inia mbali na watu; uharakisha kwenda na kurudi.
5Kwa nchi, kizalishwapo chakula, inapinduliwa kama kwa moto.
6Mawe yake yana johari, na vumbi lake lina dhahabu.
7Hata ndege mwindaji hapajui, wala jicho la kipanga halijapaona.
8Ndege mwenye majivuna hajawai kuiona njia hiyo, wala simba mkali kupita pale.
9Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake.
10Huweka njia katika miamba; macho yake pale kila kilicho cha thamani.
11Hufunga vyanzo hata wasiondoke; kilichofichika pale hukifunua.
12Hekima itakuwa wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
13Mtu hafahamu thamani yake; wala haipatikani katika nchi ya walio hai.
14Vilindi vya maji chini ya nchi husema, 'Haiko kwangu'; bahari husema, 'Haipo pamoja nami.'
15Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha.
16Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari.
17Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi.
18Hailinganishwi na marijani wala yaspi; hakika, thamani ya hekima inapita madini ya rubi.
19Topazi ya Ethiopia hailinganishwi nayo; wala kuthamanishwa kwa dhahabu safi.
20Je hekima inatoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
21Hekima imejificha mbali na macho ya viumbe wote na ndege wa angani.
22Mauti na uharibifu husema, 'Tumesikia tu tetesi kwa masikio yetu.'
23Mungu hufahamu njia ya kuipata; anapafahamu ilipo.
24Kwani uona miisho yote ya dunia na huona chini ya mbingu zote.
25Hapo kale, alifanya nguvu za upepo na kuyagawanya maji kwa kipimo.
26Aliiwekea mvua tamko na njia ya radi na munguromo.
27Kisha akaiona hekima na kuitangaza; aliianzisha, bila shaka, na kuipima.
28Aliwambia watu, 'Tazameni, kumcha Bwana - ni hekima; kuacha uovu ni ufahamu.”