18 Mungu ambaye humwambia mfalme, 'Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?
19 Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
20 Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
21 Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
22 Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
23 Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
24 Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
25 Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
26 Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
27 kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
28 Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
29 Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
30 ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
31 Fikiria mtu akimwambia Mungu, 'Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
32 nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
33 Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
34 Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,