Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi? Je siku zake si kama siku za mwajiriwa?
2Kama mtumwa atamaniye sana kivuli cha jioni, kama mwajiriwa atafutaye ujira wake -
3hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku.
4Hapo nilalapo chini, najiuliza mwenyewe, 'Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?' Nimejawa na kujitupa huku na huko hadi mwanzo wa siku.
5Mwili wangu umevikwa minyoo na madonda yenye vumbi; maumivu katika ngozi yangu yamekuwa magumu na kisha hutoweka na huendelea tena.
6Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia; zinapita bila tumaini.
7Mungu, anakumbuka kwamba maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona mema tena.
8Jicho lake Mungu, huyo anionaye mimi, halitaniangalia tena; Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako.
9kama vile wingu liishavyo na kutoweka, hivyo wale waendao sheoli hawatarudi tena kabisa.
10Yeye hatarudi tena nyumbani kwake, wala mahali pake hapatamtambua tena.
11Kwa sababu hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitasema juu ya maumivu makubwa ya roho yangu; Nitanung'unika juu ya uchungu wa nafsi yangu.
12Je mimi ni bahari au kiumbe cha kutisha baharini hata ukaweka mlinzi juu yangu?
13Hapo nisemapo, 'kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu,'
14halafu unitishapo kwa ndoto na kunitisha kwa maono,
15ili nichague kunyongwa na kufa kuliko kulinda mifupa yangu hii.
16Ninayachukia kabisa maisha yangu; sitamani siku zote kuwa hai; usinisumbue maana siku zangu hazifai.
17Je mtu ni nini hata ukatia bidii kwake, na ukaweka akili yako kwake,
18na kumwangalia kila asubuhi, na kumjaribu kila mara?

19Je itachukuwa muda gani kabla hujaacha kuniangalia, wala kunisumbua muda wa kutosha kwaajili ya kumeza mate yangu?
20Hata kama nimefanya dhambi, itakusaidia nini, wewe ulindaye wanadamu? Kwa nini umenifanya shabaha yako, kiasi kwamba nimekuwa mzigo kwako?
21Kwa nini hunisamehi makosa yangu na kuniondolea uovu wangu? kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; na wewe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwako.”