1Kwahiyo sasa, nakuomba wewe, Ayubu, usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote.
2Tazama sasa, nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu.
3Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu; yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.
4Roho ya Mungu imeniumba; pumzi ya Mwenye nguvu imenipatia uhai.
5Kama unaweza, nijibu; weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame.
6Tazama, niko kama wewe ulivyo mbele za Mungu; nimeumbwa pia kutoka katika udongo.
7Ona, tishio langu halitakufanya wewe uogope; wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.
8Umesema kwa hakika katika masikio yangu; nimeisikia sauti ya maneno yakeo yakisema,
9'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.
10Tazama, Mungu huona nafasi za kunishambulia mimi; huniangalia mimi kama adui yake.
11Huweka miguu yangu akiba; naye huangalia njia zangu zote.'
12Tazama, katika hili hauko sawa, nitakujibu, kwa kuwa Mungu ni mkuu kuliko mtu.
13Kwanini unashindana naye? Huwa hahesabu matendo yake yoyote.
14Kwa kuwa Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili, ingawa mwanadamu hawezi kutambua.
15Katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani -
16basi Mungu hufungua masikio ya watu, na kuwatisha kwa vitisho,
17kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.
18Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.
19Mtu huadhidibiwa pia na maumivu kitandani mwake, na maumivu makali yanayodumu katika mifupa yake,
20ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri.
21Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania.
22Hakika, roho yake inasogea shimoni, na uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.
23Lakini kama kuna malaika anayeweza kuwa mpatanishi kwa ajili yake, mpatanishi mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika, kumwonesha kile kilicho cha haki ili atende haki,
24na kama malaika ni mpole kwake na kumwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake,'
25kisha mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto, atazirudia siku za nguvu za ujana wake.
26Atamwomba Mungu, na Mungu atakuwa mwema kwake, ili kwamba auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha. Mungu atampa mtu ushindi wake.
27Ndipo mtu huyo ataimba mbele ya watu wengine na kusema, 'Nilitenda dhambi na kuasi kile kilichokuwa cha haki, lakini dhambi yangu haikuadhibiwa.
28Mungu ameiokoa roho yangu isiende chini shimoni; maisha yangu yataendelea kuuona mwanga.'
29Tazama, Mungu hufanya mambo haya yote pamoja na mwanadamu, mara mbili, naam, hata mara tatu,
30kuirudisha roho yake kutoka shimoni, ili kwamba aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.
31Ayubu, zingatia na unisikilize mimi; nyamaza nami nitasema.
32Ikiwa una kitu cha kusema, na unijibu; sema, maana nataka kuhakikisha kwamba wewe uko katika haki.
33Kama sivyo, basi nisikilize, ubaki kimya, nami nitakufundisha wewe hekima.”