1Ndipo Sofari, Mnaamathi alijibu na kusema,
2“Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.
3Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi, lakini roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.
4Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale, wakati Mungu alipomweka mwanadamu juu ya nchi:
5ushindi wa mtu mwovu ni mfupi, na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?
6Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu, na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu,
7bado mtu huyo atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe; wale waliokuwa wamemuona yeye watasema, 'Yuko wapi yeye'?
8Yeye atapaa mbali kama ndoto na hataonekana; ndivyo ilivyo, yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la
9usiku. Jicho ambalo lilimuona yeye halitamuona yeye tena; mahali pake hapatamuona yeye tena.
10Watoto wake wataomba msamaha kwa watu maskini, mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.
11Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani, lakini zitalala naye chini katika mavumbi.
12Japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake yeye, japokuwa yeye anauficha chini ya ulimi wake yeye,
13japokuwa anaushikilia pale na hauruhusu kwenda lakini bado huushikilia katika mdomo wake yeye -
14chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu; hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.
15Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.
16Yeye atamumunya sumu ya majoka; ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.
17Yeye hatafurahia vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.
18Yeye atayarudisha matunda ya kazi yake na hataweza kuyala; yeye hatafurahia utajiri alioupata kwa biashara zake yeye.
19Kwa kuwa yeye amewakandamiza na kuwasahau watu maskini; yeye kwa uonevu, amezichukua mbali nyumba ambazo hakuzijenga yeye.
20Kwa sababu yeye mwenyewe hakujua utoshelevu wowote, yeye hataweza kuokoa kitu chochote katika kile ambacho alijifurahisha.
21Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza; kwa hiyo mafanikio yake yeye hayatakuwa ya kudumu.
22katika wingi wa utajiri wake yeye ataanguka katika mahangaiko; mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.
23Wakati akiwa katika kulijaza tumbo lake, Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye; Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye wakati yeye anakula.
24Ingawa mtu huyo atakimbia kutoka katika silaha ya chuma, upinde wa shaba utampiga yeye.
25Mshale utatoboa kupitia mgongoni mwake na utatokezea; ni dhahiri, ncha inayong'ra itatokezea nje kupitia ini lake yeye; watesi huja tena juu yake.
26Giza lliilo kamilika limetunzwa kwa akiba zake; moto usiopulizwa utamla yeye kwa haraka; utameza kile kilichoachwa katika hema yake.
27Mbingu zitauweka wazi uovu wake, na nchi itainuka juu dhidi yake yeye kama shahidi.
28Utajiri wa nyumba yake utatoweka; bidhaa zake zitamwagika mbali siku ya ghadhabu ya Mungu.
29Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu, urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye.”