Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2“kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
3Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
4Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
5ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
6ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
7Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
8ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
9ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
10Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
11Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
12Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
13Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
15Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
16Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
17kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
18Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.

19Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
20Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
21Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
22Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
23Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
24Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
25Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
26Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
27Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
28Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
29Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
30Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
31Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
32Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
33Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
34Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
35Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.