Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema,
2“Je, lini utaacha kusema kwako? Fikiri, na baadaye tutazungumza.
3Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama mwitu; kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako?
4Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako, nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?
5Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra.
6Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa nje.
7Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi; mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini.
8Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko.
9Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake.
10Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia.
11Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote; wao watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake.
12Utajiri wake utageuka kuwa njaa, na majanga yatakuwa tayari upande wake.
13Sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa; Hakika, mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye.
14Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake na hakuweza kutembea kwenda kwa mfalme mwenye utisho.
15Watu ambao siyo wa kwake wataishi kwenye hema yake baada ya kuona ule moto mesambaa ndani ya nyumba yake yeye.
16Mizizi yake itanyauka chini yake; juu tawi lake yeye litakatwa.
17Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa.
18Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu.

19Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa.
20Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho.
21Hakika hizo ni nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu.”