Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Je unajua ni wakati gani mbuzi mwitu huzaa watoto wao katika miamba? Je waweza kuwangalia paa wakati wanapozaa watoto wao?
2Waweza kuhesabu miezi ya kuchukua mimba? Je unaujua muda ambao huzaa watoto wao?
3Wanainama chini na kuzaa watoto wao, na kisha maumivu yao ya uzazi yanaishi.
4Watoto wao huwa na nguvu na kukua katika uwanda wa wazi; hutoka nje na hawarudi tena.
5Ni nani huwaacha punda mwitu waende huru? Je nani amevilegeza vifungo vya punda wepesi,
6ni nyumba ya nani nimeifanya katika Araba, au nyumba yake katika nchi ya chumvi?
7Hucheka kwa dharau katika kelele katika mji; hasikilizi kelele za mwongozaji.
8Hutembeatembea juu ya milima kama malisho yake; huko hutafuta kila mmea ulio wa kijani kwa ajili ya kula.
9Je nyati atakuwa na furaha kukutumikia? Je atakubali kukaa katika zizi lako?
10Waweza kumwongoza nyati kulima mtaro kwa kamba? Je atachimba bonde kwa ajili yako?
11Je waweza kumtumaini kwasababu ya nguvu zake nyingi? Je waweza kumwachia kazi yako ili aifanye?
12Je waweza kumtegemea akuletee nyumbani nafaka, au kukusanya nafaka katika uwanda wako wa kupuria?
13Mabawa ya mbuni hupunga kwa majivuno, bali je mabawa na manyoya yana upendo?
14Kwa maana huuacha mayai yake katika nchi, na huyaacha yapate joto katika mavumbi;
15husahau kuwa mguu waweza kuyaharibu au kwamba mnyama mwitu aweza kuyakanyaga.
16Huyatendea vibaya makinda yake kana kwamba si yake; haogopi kwamba kazi yake yaweza kupotea bure,
17kwasababu Mungu amemnyima hekima na hajampa ufahamu wowote.
18Na wakati anapokimbia kwa haraka, huwacheka kwa dharau farasi na mpanda farasi wake.

19Je umempa farasi nguvu zake? Je umeivika shingo yake kwa manyoya?
20Je umemfanya aruke kama panzi? Enzi ya mlio wake ni wa kutisha.
21Hurarua kwa nguvu na kufurahia katika nguvu zake; hukimbia upesi kukutana na silaha.
22Huidharau hofu na hashangazwi; huwa harudi nyuma kutoka katika upanga.
23Podo hugongagonga ubavuni mwake, pamoja na mkuki unaong'aa na fumo.
24Huimeza nchi kwa hasira na ghadhabu; katika sauti ya tarumbeta, hawezi kusimama sehemu moja.
25Wakati wowote tarumbeta inapolia, husema, 'Ooh! Huisikia harufu ya vita kutoka mbali - vishindo vya radi za makamanda na makelele.
26Je ni kwa hekima yako kwamba mwewe hupaa juu, na ya kuwa huyanyosha mabawa yake kwa upande wa kusini?
27Je ni kwa agizo lako kwamba tai huruka juu na kufanya kiota chake katika sehemu za juu?
28Huishi katika majabali na hufanya makao yake katika vilele vya majabali, na ngomeni.
29Kutoka huko hutafuta mawindo; macho yake huyaona mawindo kutoka mbali.
30Makinda yake hunywa damu pia; na pale walipo watu wafu, ndipo na yeye alipo.