Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Roho yangu imemezwa, na siku zangu zimekwisha; kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi.
2Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami; ni lazima daima jicho langu litazame kukasirisha kwao.
3Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe; nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi?
4Kwa kuwa wewe Mungu umemeitunza mioyo yao kutoka katika ufahamu; kwa hiyo, wewe hautawaheshimisha wao juu yangu mimi.
5Yeye ambaye huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
6Lakini amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu; wao wananitemea mate katika uso wangu mimi.
7Jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni; sehemu zangu zote za mwili ni nyembamba kama vivuli.
8Watu wanyoofu watapendezwa na hiki; mtu asiye na hatia atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi ya watu wasiomcha Mungu.
9Mtu mwenye haki ataendelea katika njia yake; yeye ambaye ana mikono iliyo safi ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi.
10Lakini kama ilivyo kwenu ninyi nyote, njooni sasa; Mimi sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu ninyi.
11Siku zangu zimepita; mipango yangu imenyamazishwa na hivyo ni matumaini ya moyo wangu.
12Watu hawa, wenye kukejeli, badili usiku kuwa mchana; mchana uko karibu kuwa giza.
13Tangu mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu; tangu Mimi nimetandaza kiti changu katika giza;
14tangu Mimi nimesema na shimo 'Wewe ni baba yangu,' na kwa funza, 'Wewe ni mama yangu au dada yangu;
15liko wapi tena tumaini langu? Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote?
16Tumaini litakwenda pamoja na mimi katika milango ya Kuzimu wakati sisi tutakapokwenda katika mavumbi?