1Ita sasa; je kuna yeyote ambaye atakujibu? Utamrudia yupi katika watakatifu hao?
2Kwa kuwa hasira huua mtu mpumbavu; wivu huua mjinga.
3Nimemuona mtu mpumbavu akishika mzizi, lakini ghafla niliyalaani makazi yake.
4Watoto wake wako mbali na uzima; wameangamia langoni mwa mji. Hakuna yeyote atakaye waponya.
5Mwenye njaa hula mavuno yao; hata huyachukua katikati ya miiba. Wenye kiu huzihemea mali zao.
6Kwa kuwa magumu hayatoki udongoni; wala taabu haichipuki katika nchi.
7Badala yake, wanadamu huzaliwa kwaajili ya taabu, kama tu cheche za moto zirukavyo juu.
8Lakini kwa mimi, ningemrudia Mungu mwenyewe; kwake ningeaminisha kusudi langu -
9yeye afanyae makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu.
10Hutoa mvua juu ya nchi, na huyapeleka maji mashambani.
11Hufanya haya kwaajili ya kuwainua juu hao walio chini; huwapandisha sehemu salama hao waombolezao.
12Yeye huharibu mipango ya watu wenye hila, ili mikono yao isipate mafanikio.
13Yeye huwanasa watu wenye hekima katika matendo ya hila zao wenyewe; mipango ya watu waliogeuzwa huharibika haraka.
14Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, na hupapasa mchana kama vile ni usiku.
15Lakini yeye huokoa maskini kwa upanga wa vinywa vyao na mhitaji kwa mkono wa mtu mwenye nguvu.
16Hivyo mtu maskini ana matumaini, na udhalimu hufumba kinywa chake mwenyewe.
17Tazama, amebarikiwa mtu ambaye hutiwa adabu na Mungu; kwa sababu hiyo, usidharau uongozi wa Mwenyezi.
18Kwa kuwa yeye hujeruhi na kisha huuguza; yeye hutia jeraha na kisha mikono yake huponya.
19Yeye atakuokoa na mateso sita; kweli, katika mateso saba, hakuna uovu utakao kugusa.
20Wakati wa njaa atakukomboa na kifo, na kwa uwezo wa upanga wakati wa vita.
21Wewe utafichwa na mateso ya ulimi; na usitishike na uharibifu utakapokuja.
22Wewe utaufurahia uharibifu na njaa, na hutatishika na wanyama wakali wa nchi.
23Kwa kuwa wewe utakuwa na mapatano na mawe ya shambani mwako, na wanyama wa mwituni watakuwa na amani na wewe.
24Wewe utajua kwamba hema lako lina usalama; utatembelea zizi la kondoo wako na hutakosa kitu chochote.
25Pia utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, na vizazi vyako vitakuwa kama nyasi ardhini.
26Wewe utafika kaburini kwako mwenye umri kamili, kama vile rundo la mashuke ya nafaka liendavyo juu wakati wake.
27Tazama, tumelipeleleza jambo hili; ndivyo lilivyo; lisikie, na ulifahamu kwa ajili yako mwenyewe.”