Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 38

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo Yahweh alimwita Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kumwambia,
2“Huyu ni nani aletaye giza katika mipango kwa njia ya maneno bila maarifa?
3Basi sasa jifunge kiunoni mwako kama mwanaume kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
4Wewe ulikuwa wapi wakati nilipoitandaza misingi ya dunia? Niambie, kama unao ufahamu zaidi.
5Je ni nani aliyeamuru vipimo vyake? Niambie, kama unajua, ni nani alivinyosha vipimo juu yake?
6Misingi yake ilitandazwa juu ya nini? Ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni
7wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8Ni nani huifunga bahari kwa milango wakati inapofurika, kana kwamba inatoka katika tumbo,
9wakati nilipoyafanya mawingu kuwa ni mavazi yake, na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia?
10Hapo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu, na nilipoweka makomeo yake na milango,
11na wakati nilipoiambia, 'Unaweza kuja hapa kutoka mbali, lakini si zaidi; na hapa ndipo nitauweka mpaka kwa fahari ya mawimbi yako.'
12Je tangu mwanzo wa siku zako, ulishawahi kuigiza asubuhi ianze, na kuyafanya mapambazuko yajue sehemu yake katika mpangilio wa vitu,
13ili kwamba ishikilie sehemu za dunia ili watu waovu watikiswe mbali nayo.
14Dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhuri; vitu vyote husimama juu yake dhahiri kama cha kibindo cha nguo.
15'Mwanga' wao umeondolewa kutoka kwa watu waovu; na mkono wao ulioinuliwa umevunjwa.
16Je umeshaenda kwenye vyanzo vya maji ya bahari? Je umeshatembea sehemu za chini kabisa za kilindi?
17Je malango ya mauti yamefunuliwa kwako? Je umeshaona malango ya uvuli wa mauti?
18Je umeifahamu dunia katika upana wake? Niambie kama unayajua yote hayo.

19Je iko wapi njia ya sehemu ya kupumzikia kwa mwanga, na kama ilivyo kwa giza, iko wapi sehemu yake?
20Je unaweza kuuongoza mwanga na giza katika sehemu zake za kazi? Waweza kuitambua njia ya kurudi katika nyumba zao?
21Bila shaka unajua, kwa kuwa ulizaliwa wakati huo; hesabu ya siku zako ni kubwa sana!
22Je ulishaingia katika ghala ya barafu, au umeshaiona ghala ya mawe ya mvua,
23vitu hivi nimeviweka kwa ajili ya siku za mateso, kwa siku za mapigano na vita?
24Je iko wapi njia ya mshindo wa mwanga hutokea au je upepo husambazwa kutoka mashariki juu ya dunia?
25Ni nani aliyezitengeneza mifereji ya gharika ya mvua, au ni nani aliyezifanya njia za milipuko ya radi,
26na kuifanya mvua inyeshe juu ya nchi ambazo hakuna mtu aishiye ndani yake, na juu ya jangwa, ambayo ndani yake hakuna mtu yeyote,
27kwa kusudi la kutimiza mahitaji ya mikoa iliyo kame na yenye ukiwa, na kuyastawisha majani mororo?
28Je kuna baba wa mvua? Ni nani aliyeyafanya matone ya umande?
29Je barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na ni nani aliyeizaa theluji nyeupe katika anga?
30Maji hujificha menyewe na kuwa kama jiwe; sehemu za juu za vilindi huwa kama barafu.
31Je unaweza kuzifunga minyororo ya Kilimia, au kuvifungua vifundo vya Orioni?
32Je unaweza kuziongoza nyota kutokea katika nyakati zake? Je waweza kuongoza dubu pamoja na watoto wake?
33Je unazijua sheria za anga? Wewe uliweza kuanzisha sheria za anga juu ya dunia?
34Je waweza kupaza sauti yako hadi mawinguni, ili kwamba maji mengi ya mvua yakufunike?
35Je waweza kuagiza miali ya mwanga ili itokee, na kukwambia, 'Sisi tupo hapa'?
36Ni nani ameweka hekima katika mawingu au ni nani ameweka ufahamu kwa ukungu?

37Nani anaweza kuyahesabu mawingu kwa maarifa yake? Na ni nani awezaye kuvimwaga viriba vya anga
38wakati mavumbi yanapoungana kuwa kitu kigumu na mabonge ya dunia yanaposhikama kwa pamoja?
39Je waweza kuwinda mawindo kwa ajili ya simba jike au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba
40wakati wanapokwaruza kwaruza katika pango lao na kukaa katika kificho ili kulala katika hali ya kuvizia?
41Ni nani aletaye mawindo kwa ajili ya kunguru wakati ambapo watoto wao wanapomlilia Mungu na kutangatanga kwa kukosa chakula?