1Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, huishi siku chache tu na amejaa mahangaiko.
2Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu.
3Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi?
4Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote.
5Siku za mwanadamu zimeamriwa. Idadi ya miezi yake unayo wewe; umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka.
6Tazama mbali kutoka kwake kwamba yeye aweze kupumzika, ili kwamba aweze kufurahia siku yake kama mtu aliyekodishwa kama yeye anaweza kufanya hivyo.
7Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti; kama ukikatwa chini, unaweza kuchipua tena, hivyo chipukizi lake halitapotea.
8Japokuwa mizizi yake inakua na kuzeeka katika ardhi, na shina lake kufa katika udongo,
9hata kama bado lina harufu ya maji pekee, litachipua tena na kutoa nje matawi kama mche.
10Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye?
11Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka,
12vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.
13Laiti, kwamba ungenificha mimi mbali katika kuzimu mbali kutoka katika mahangaiko, na kwamba ungenitunza mimi katika siri hadi hasira yake imalizike, kwamba ungeniwekea mimi muda maalumu wa kukaa huko na kisha kuniita mimi katika fahamu!
14Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena? Ikiwa hivyo, ningependa kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja.
15Wewe ungeita, na mimi ningekujibu wewe. Wewe ungekuwa na shauku ya kazi ya mikono yako.
16Wewe ungehesabu na kutunza nyayo zangu; Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu.
17Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba; wewe ungeufunga uovu wangu.
18Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake;
19maji yaliyokuwa chini ya mawe; kufurika kwake huondoa mbali mavumbi ya nchi. Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu.
20Ninyi daima humshinda yeye, na yeye hupita mbali; Ninyi mnabadilisha uso wake na kumtuma yeye mbali kufa.
21Kama watoto wake wa kiume ni wa kuheshimiwa, yeye, hatambui hicho; na kama wakishushwa chini, yeye haoni hicho.
22Yeye hujisikia tu maumivu ya mwili wake mwenyewe, na hujiombolezea yeye mwenyewe.