Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija?
2Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao.
3Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana.
4Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao.
5Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao.
6Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu.
7Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi.
8Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao.
9Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini.
10Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula.
11Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu.
12Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao.
13Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake.
14Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku.
15Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha.
16Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru.
17Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro.
18Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu.

19Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi.
20Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti.
21Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane.
22Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha.
23Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao.
24Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka.
25Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?”