Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Elihu aliendelea na kusema,
2“Niruhusu niseme kidogo zaidi, nami nitakuonesha baadhi ya mambo kwasababu nina maneno machache ya kusema kwa ajili ya Mungu.
3Nitapata maarifa yangu kutoka mbali; nitatambua kwamba haki ni ya Muumba wangu.
4Kwa kweli, maneno yangu hayatakuwa ya uongo; mtu fulani aliyekomaa katika maarifa yu pamoja nawe.
5Angalia, Mungu ni mwenye nguvu, na hamdharau mtu yeyote; yeye ni mwenye nguvu katika uweza wa ufahamu.
6Yeye huwa hayahifadhi maisha ya watu waovu bali badala yake hufanya yaliyo ya haki kwa wale wanaoteseka.
7Haondoi macho yake kwa wenye haki bali badala yake huwaweka juu ya viti vya enzi kama wafalme milele, nao wameinuliwa juu.
8Ikiwa wamefungwa minyororo na kunaswa katika kamba za mateso,
9kisha huwafunulia kile walichokifanya, na maovu yao na kiburi chao.
10Hufungua pia masikio yao kwa ajili ya agizo lake, na huwaamuru wageuke kutoka katika uovu.
11Ikiwa watamsikiliza na kumwabudu yeye, wataishi katika mafanikio katika siku zao, na miaka yao katika hali ya kuridhika.
12Hata hivyo, kama hawatasikiliza, wataangamia kwa upanga; watakufa kwasababu hawana maarifa.
13Na wale wasiomjua Mungu hutunza hasiria zao katika mioyo; hawaombi msaada hata wakati ambapo Mungu huwafunga.
14Hawa hufa katika ujana wao; na maisha yao hukoma kati ya makahaba.
15Mungu huwainua watu walioonewa kwa njia ya mateso yao; hufungua masikio yao kwa njia ya uonevu wao.
16Kwa hakika, yeye angependa kuwatoa ninyi katika mateso na kuwaweka katika sehemu pana ambapo hakuna masumbufu na mahali ambapo meza yenu ingewekwa ikiwa na chakula kilichojaa mafuta.
17Lakini wewe umejaa hukumu juu ya watu waovu; hukumu na haki umeziachilia.
18Usiuache utajiri ukuvute katika udanganyifu; na sehemu kubwa ya rushwa isikugeuze upande kutoka katika haki.

19Je utajiri wako waweza kukunufaisha, ili kwamba usiwe katika taabu, au nguvu zako zote za uwezo zaweza kukusaidia?
20Usiutamani usiku ili utende dhambi dhidi ya wengine wakati ambapo mataifa hukatiliwa mbali katika nafasi zao.
21Uwe mwangalifu ili kwamba usigeukie dhambi kwasababu unajaribiwa kwa mateso ili kwamba ukae mbali na dhambi.
22Angalia, Mungu ameinuliwa katika nguvu zake; ni nani aliye mwalimu kama yeye?
23Ni nani alishamwalekeza njia yake? Nani anayeweza kumwambia, 'Wewe umetenda mambo yasiyo ya haki?'
24Kumbuka kuyasifu matendo yake, ambayo watu wameyaimba.
25Watu wote wameshayatazama hayo matendo, lakini wanayaona tu matendo hayo kwa mbali sana.
26Tazama, Mungu ni mkuu, lakini sisi hatumfahamu yeye vizuri; hesabu ya miaka yake haihesabiki.
27Kwa kuwa yeye huvuta matone ya maji ili kuyachuja kama mvua katka mvuke wake,
28ambayo mawingu yake huyamwaga chini na kuyandondosha kwa wingi kwa mwanadamu.
29Hakika, kuna hata mmoja awezaye kuelewa kwa undani kusambaa kwa mawingu na radi kutoka katika nyumba yake?
30Angalia, hueneza mwanga wake kumzunguka na kufunika mizizi ya bahari.
31Kwa namna hii huyahukumu mataifa na kuwapa chakula kwa wingi.
32Yeye huuijaza mikono yake kwa mwanga mpaka pale anapouamuru kupiga shabaha yake.
33Na muungurumo wake huonya kwa dhoruba, wanyama wanaweza kusikia kuja kwake.