Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2“Mimi nimevisikia vitu hivyo vingi; ninyi nyote ni wafariji wenye kuhuzunisha.
3Maneno yenye upuuzi daima yanaweza kuwa na mwisho? Nini kimeharibika kwenu kwamba mnajibu kama hivi?
4Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi mnavyofanya, kama ninyi mngekuwa katika nafasi yangu; Mimi ningekusanya na kuunganisha maneno pamoja dhidi yenu na kutikisa kichwa changu kwenu ninyi katika dhihaka.
5Laiti, jinsi gani Mimi ningewatia moyo na midomo yangu! Jinsi gani faraja kutoka midomo yangu ingenga'risha huzuni yenu!
6Ikiwa Mimi ninazungumza, kuomboleza kwangu hakujasikilizwa; Ikiwa nikiendelea katika kuzungumza, jinsi gani mimi ninaidiwa?
7Lakini sasa, Mungu,
8wewe umenifanya mimi kuchoka; wewe umeifanya familia yangu yote kuwa ukiwa. Wewe umenifanya mimi kukauka, ambayo yenyewe ni ushuhuda dhidi yangu mimi; kukonda kwa mwili wangu huinuka dhidi yangu, na kunashuhudia dhidi ya macho yangu.
9Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande.
10Watu wameachama na midomo iliyowazi juu yangu; wamenipiga mimi katika shavu kwa kunitukana; wamekusanyika pamoja kinyume changu mimi.
11Mungu amenikabidhi mimi juu ya watu wasio mcha Mungu, na kunitupa mimi ndani ya mikono ya watu waovu.
12Mimi nilikuwa katika wepesi, na yeye amenivunjavunja mimi vipande. Hakika, amenichukua mimi kwa shingo na ameniponda mimi vipande vipande; yeye pia ameniweka mimi juu kama shabaha yake.
13Wapiga upinde wake wote wamenizunguka mimi; Mungu huzikata vipande vipande figo zangu, na haniokoi mimi; yeye humwaga nje nyongo yangu juu ya ardhi.
14yeye hukanyaga kanyaga kupitia ukuta wangu tena na tena; yeye hukimbia juu yangu mimi kama shujaa.
15nguo ya magunia juu ya ngozi yangu; Mimi nimeisukuma kwa nguvu pembe yangu ndani ya ardhi.
16Uso wangu ni mwekundu na kuomboleza; juu ya ngozi inayofunika macho kuna kivuli cha mauti
17ingawa hakuna dhuluma katika mikono yangu, na kuomba kwangu ni safi.
18Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi; acha kulia kwangu kuwe hakuna mahali pa kupumzika.

19Hata sasa, tazama, ushuhuda wangu uko mbinguni; yeye ambaye ashuhudiaye kwa ajili yangu mimi yuko juu.
20Rafiki zangu wananicheka kwa dharau, lakini jicho langu linamwaga machozi kwa Mungu.
21Mimi ninaomba ule ushuhuda ulioko mbinguni kumtetea mtu huyu na Mungu kama mwanadamu afanyavyo na jirani yake.
22Kwa maana wakati miaka michache itakapokuwa imepita, Mimi nitakwenda mahali ambapo mimi sitaweza kurudi.