1Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2“Mmemsaidiaje aliyedhaifu!
3Jinsi gani mmemshauri asiye na hekima na kutamka maneno yenye maarifa kwake!
4Kwa msaada wa nani mmesema maneno haya? Ni roho ya nani iliyotoka ndani yenu?
5Maiti inatetemeka chini ya maji, na vyote wilivyomo ndani yake.
6Kuzimu kuko wazi mbele ya Mungu; uharibifu hauna kizuizi dhidi yake.
7Huitandaza kaskazi juu ya nafasi wazi na kuining'iniza dunia hewani.
8Huyafunga maji katika mawingu yake mazito, lakini hayagawanyiki chini yake.
9Huufunika uso wa mwezi na kueneza mawingu yake juu yake.
10Amechora ukingo wa duara juu ya maji kama mpaka kati ya nuru na giza.
11Nguzo za mbinguni zinatikisika na zimestushwa na kukemea kwake.
12Aliituliza bahari kwa uwezo wake; kwa ufahamu wake alimwaribu Rahab
13Kwa pumzi yake, aliziondoa mbingu kwa dhorubu; mbingu ziliondolewa kwa dhorubu; mkono wake ulimchoma nyoka anayekimbia.
14Tazama, hizi si zaidi ya madogo ya njia zake; Jinsi gani tunasikia akitunong'oneza! Ni nani awezaye kufahamu uwezo wake.