Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema,
2“Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni.
3Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake?
4Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye?
5Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake.
6Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!”