Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baada ya hayo, Ayubu akafunua kinywa chake na kuilani siku aliyozaliwa.
2Akasema,
3“Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
4Siku hiyo na iwe giza; Mungu toka juu asiifikilie, wala mwanga usiiangazie.
5Ishikwe na giza na giza la mauti liwe lake. Wingu na likae juu yake; kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza kweli na kiitishe.
6Usiku huo, na ukamatwe na giza tororo. Usihesabiwe miongoni mwa siku za mwaka; na usiwekwe katika hesabu ya miezi.
7Tazama, usiku huo na uwe tasa; na sauti ya shangwe isiwe ndani yake.
8Na wailani siku hiyo, hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathani.
9Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza. Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate; wala makope ya mapambazuko isiyaone,
10kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu, na kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.
11Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi? Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?
12kwanini magoti yake yalinipokea? Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?
13Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimya kimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko
14pamoja na wafalme na washauri wa dunia, ambao walijijengea makaburi ambayo sasa ni magofu.
15Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha.
16Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.
17Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.
18Huko wafungwa kwa pamoja hupata amani; hawaisikii sauti ya msimamizi wa watumwa.

19Wote wadogo na watu maarufu wako huko; mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.
20Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai,
21ambao hutamani mauti lakini hawapati; ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika?
22Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi?
23Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa?
24Kwa kuwa kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji.
25Maana jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia.
26Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko; badala yake huja taabu.”