Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Aidha, Elihu aliendelea kusema,
2“Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
3Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
4Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
5Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
6Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
7Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
8Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
9Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
10Lakini hakuna hata mmoja asemaye, 'Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
11ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
12Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
13Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
14Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
15Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
16Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa.”