Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
2Kama mtu yeyote akijaribu kuzungumza na wewe, je utakosa ustahimilivu? Lakini ni nani anaweza kujizuia asizungumze?
3Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
4Maneno yako yamemsaidia yeye mwanamme aliyekuwa anaanguka; wewe umeyaimarisha magoti dhaifu.
5Lakini sasa matatizo yamekuja kwako, na wewe umechoka; yanakugusa wewe, na wewe umetatizika.
6Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?
7Tafakari juu ya hili, tafadhari: ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa? Au ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali?
8Kutokana na vile nilivyoona, wale walimao uovu na kupanda taabu huvuna hayo.
9Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea.
10Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.
11Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
12Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo.
13Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu.
14Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika.
15Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama.
16Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
17“Je binadamu anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu? Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko muumba wake?
18Tazama, kama Mungu hawaamini watumishi wake; kama hulaumu upumbavu wa malaika zake,

19je si zaidi sana ukweli huu kwa wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi, wale waliopondwa mbele ya nondo?
20Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa; wameangamia milele wala bila yeyote kuwatambua.
21Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Wanakufa; wanakufa bila hekima.