Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ayubu akaendelea kuoengea na kusema,
2“Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu,
3kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu.
4Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo.
5Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu.
6Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi.
7Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki.
8Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake?
9Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat?
10Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote
11Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi.
12Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana.
13Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi.
14Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa.
15Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea.
16Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi,
17na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali.
18Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi.

19Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu.
20Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku.
21Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake.
22Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake.
23Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.