Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2“Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
3Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
4Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
5Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
6Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
7Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
8Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
9Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
10Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
11Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
12Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
13Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
14Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
15Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
16Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
17Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.