Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ayubu akaendelea na kusema,
2Ee, ningekuwa kama nilivyokuwa miezi iliyopita wakati Mungu aliponiagalia,
3taa yake ilipowaka kichwani pangu, na pale nilipotembea gizani kwa nuru yake.
4Ee, kwamba ningekuwa kama nilivyokuwa katika siku za ujana wangu uhusiano wangu na Mungu ulivyokuwa mzuri,
5wakati Mwenyezi alipokuwa pamoja nami, na wanangu walipokuwa karibu nami,
6wakati maisha yangu yalipokuwa yamejawa na utele, na mwamba uliponichuruzishia chemichemi za mafuta.
7Nilipokwenda langoni mwa mji, nilipokaa katika eneo la mji,
8vijana waliniona na walikaa mbali kwa kuniheshimu, na wazee waliinuka na kusimama kwa ajili yangu.
9Wana wa mfalme waliacha kuongea nilipofika; wangeweka mkono wao katika vinywa vyao.
10Sauti za waheshimiwa zililazimishwa, na ndimi zao hazikuweza kuongea vinywani mwao.
11Kwani baada ya kunisikia, wangenibariki; waliponiona, wangeniona na kuniheshimu
12kwa maana nilikuwa nikiwasaidia masikini waliokuwa wakiteseka, na yatima, asiye na msaada.
13Baraka zao waliokuwa karibu kuangamia zilinipata; niliufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14Nilijivika utakatifu, nao ulinifunika; haki yangu ilikuwa kama kanzu na kilemba.
15Niliwasaidia vipofu; niliwasaidia walemavu.
16Niliwasaidia wahitaji; niliwasaidia hata wasionijua.
17Nilimnyamazisha mwovu; nilimpokonya manusura kutoka katika meno yake.
18Kisha nilisema nitakufa mahali salama; nitazizidisha siku zangu kama mchanga.

19Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu.
20Heshima yangu ni mpya daima, na nguvu za upinde wangu zipo katika mkono wangu kila wakati.
21Watu walinisikiliza; walinisubiri; walisikiliza ushauri wangu.
22Nilipo maliza kuongea hawakunena tena, maneno yangu yaliwatia nguvu kama mvua.
23Waliningoja kama kungoja mvua; waliyathamini maneno yangu, kama walivyotamani mvua iliyokawia.
24Niliwafurahia bila wao kutarajia; hawakukataa uzuri wa uso wangu.
25Nilikuwa kama mfalme wao na kuwachagulia cha kufanya; nilikuwa kama mfalme katika jeshi lake, kama awafarijiye waombolezaji mazishini.