Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Je waweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki? Au kumfunga taya zake kwa kamba?
2Je waweza kuweka kamba katika pua zake, au kumtoboa taya yake kwa ndoano?
3Je atafanya maombi mengi kwako? Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?
4Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?
5Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege? Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?
6Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara? Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?
7Je waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?
8Weka mkono wako juu yake mara moja, nawe utaikumbuka vita na hautaendelea kufanya hivyo tena.
9Tazama, matumaini ya kila mtu ambaye hufanya hivyo ni uongo; je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?
10Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba; Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?
11Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa? Chochote kilicho chini ya anga ni changu.
12Sitanyamaza kimya kuhusu miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.
13Nani awezaye kuiondoa ngozi yake? Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?
14Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?
15Mgongo wake umefanywa kwa magamba yenye mistari, yamefungwa kwa pamoja kama chapa.
16Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.
17Yameunganishwa moja kwa jingine; yamegandamana kwa pamoja, ili kwamba hayawezi kutenganishwa.
18Mwanga hung'ara kutoka katika kupumua kwake; macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi.

19Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje.
20Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.
21Pumzi yake huwasha mkaa na kuwa mwali; moto hutoka katika mdomo wake.
22Katika shingo yake kuna nguvu, na kitisho hucheza mbele yake.
23Nofu za mwili wake zimeunganishwa pamoja; ziko imara katika yeye; wala haziwezi kuondolewa.
24Moyo wake ni mgumu kama jiwe - hakika, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.
25Na anaposimama mwenyewe, hata miungu huogopa; hurudi nyuma kwasababu ya hofu.
26Na ikiwa atapigwa kwa upanga, hauwezi kumfanya kitu chochote, wala mkuki, wala mshale, wala aina yoyote ya silaha iliyochongoka.
27Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza.
28Mshale hauwezi akamfanya akimbie; kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.
29Marungu huyaangalia kama majani makavu; yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma.
30Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu; huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.
31Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto; huifanya bahari kama chungu cha lihamu.
32Yeye huifanya njia ing'are nyuma yake; mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.
33Hakuna cha kumlinganisha juu ya dunia, ambaye yeye alikuwa ameumbwa kuishi pasipo hofu.
34Hukiona kila kitu chenye kiburi; yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi.”