Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 40

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh aliendelea kuongea na Ayubu na kusema,
2“Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi? Na yeye anayehojiana na Mungu, na ajibu yeye.”
3Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema,
4“Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu.
5Ninazungumza mara moja, na sitakujibu; hakika, mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.”
6Kisha Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kusema,
7“Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume, kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
8Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki? Je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki?
9Je una mkono kama wa Mungu? Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye?
10Jivike sasa katika utukufu na katika utu; jivalie mwenyewe heshima na enzi.
11Sambaza ziada ya hasira yako; mtazame kila mmoja mwenye kiburi na umshushe chini.
12Mwangalie kila mmoja mwenye kiburi na umweke chini; wakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama.
13Wazike ardhini pamoja; zifunge nyuso zao katika sehemu zilizositirika.
14Ndipo pia nitakapokubali ya kwamba mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
15Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe.
16Ona sasa, nguvu zake ziko katika viuno vyake; nguvu zake zi katika mishipa ya tumbo lake.
17Yeye huuondoa mkia wake kama mti wa mwerezi; mishipa ya paja lake imeunganishwa pamoja.
18Mifupa yake ni kama ya mirija ya shaba; na miguu yake ni kama kipande cha chuma.

19Yeye ni mkuu wa viumbe vya Mungu. Ni Mungu pekee, ambaye alimwumba, anaweza kumshinda.
20Kwa kuwa milima humpatia chakula; hayawani wa mashambani hucheza karibu.
21Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope.
22Miti yenye vivuli humfunika katika vivuli vyake; mierebi ya kijito inamzunguka pande zote.
23Tazama, kama mto utazigharikisha kingo zake, hatikisiki; yeye anajiamini, hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake.
24Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano, au kuichoma pua yake kwa mtego?