Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 107

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mshukuruni Yahwe, maana ni mwema, na uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2Waseme hivi waliokombolewa na Yahwe, wale aliowaokoa toka mkononi mwa adui.
3Yeye amewakusanya kutoka nchi za kigeni, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.
4Walitanga-tanga janwani katika njia ya nyika hawakuona mji wa kuishi.
5Kwa sababu walikuwa na njaa na kiu, walikata tamaa kutokana na uchovu.
6Kisha walimuita Yahwe katika shida yao, naye aliwaokoa toka katika dhiki yao.
7Aliwaongoza kupitia njia ya moja kwa moja waweze kwenda mjini kuishi humo.
8Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliowatendea wanadamu!
9Maana hutosheleza shauku za walio na kiu, na hamu ya wale wenye njaa yeye huwashibisha kwa mambo mema.
10Baadhi walikaa katika giza na uvuli wa mauti, walifungwa katika mateso na minyororo.
11Hii ni kwa sababu walikuwa wameliasi neno la Mungu na walikataa maelekezo ya Aliye Juu.
12Aliinyenyekesha mioyo yao kupitia magumu; walipata mashaka na hakukuwa na mmoja wa kuwasaidia.
13Kisha wakamwita Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
14Aliwatoa gizani na kwenye uvuli wa mauti na kuvunja vifungo vyao.
15Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyoyatenda kwa wanadamu!
16Kwa maana amevunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma.
17Walikuwa wapumbavu katika njia zao za uasi na kuteswa kwa sababu ya dhambi zao.
18Walipoteza hamu yao ya kula chakula chochote, na waliyakaribia malango ya kifo.

19Kisha walimlilia Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
20Alituma neno lake na likawaponya, na akawaokoa kutoka katika uharibifu wao.
21Oh ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyoyatenda kwa wanadamu!
22Na watoe dhabihu ya shukrani na kutangaza matendo yake kwa kuimba.
23Baadhi husafiri baharini katika meli na kufanya biashara juu ya bahari.
24Hawa huona matendo ya Yahwe na maajabu yake baharini.
25Kwa maana aliamuru na alivumisha upepo wa dhoruba ambao uliyainua juu mawimbi ya baharini.
26Walipanda juu mawinguni na kushuka vilindini. Nafsi zao ziliyeyuka katika dhiki.
27Waliyumba-yumba na kupepesuka kama walevi na hawakujua la kufanya.
28Kisha walimlilia Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao.
29Aliituliza dhoruba, na mawimbi yakatulia.
30Ndipo walifurahia kwa sababu bahari ilikuwa shwali, na aliwaleta kwenye bandari waliyoitamani.
31Oh, ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyowatendea wanadamu!
32Wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu na wamsifu yeye katika baraza la viongozi.
33Aligeuza mito ikwa jangwa, chemchem ya maji ikawa nchi kame,
34na nchi ya matunda mengi ikawa nchi isiyozaa kwa sababu ya uovu wa watu wake.
35Aligeuza jangwa likawa ziwa la maji na nchi kame ikawa chemchem ya maji.
36Aliwakalisha huko wenye njaa, nao walijenga mji na kuishi humo.

37Walijenga mji ili kupanda mimea shambani, kupanda mizabibu, na kuleta humo mazao tele.
38Yeye huwabariki wameongezeka sana katika hesabu. Haachi mifugo yao ipungue katika hesabu.
39Kisha wakapungua na kudhilika kwa dhiki na mateso.
40Akawamwagia viongozi dharau na akawafanya wazunguke katika jangwa, mahali pasipo na njia.
41Lakini aliwalinda wahitaji dhidi ya mateso na kujali kwa ajili ya familia yake kama kundi la kondoo.
42Wenye haki wataona hili na kufurahi, na uovu wote utaona na kufunga kinya chake.
43Yeyote mwenye hekima anapaswa kuyaangalia haya na kutafakari juu ya matendo ya uaminifu wa agano la Yahwe.