Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 113

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe.
2Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele.
3Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe.
4Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni.
5Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu,
6atazamaye chini angani na duniani?
7Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani,
8ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
9Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!