Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 116

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nampenda Yahwe kwa kuwa anasikia sauti yangu na kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
2Kwa sababu alinisikiliza, nitamuita yeye ningali ninaishi.
3Kamba za mauti zilinizunguka, na mitego ya kuzimu ilinikabili; niliona dhiki na huzuni.
4Kisha niliita kwa jina la Yahwe: “Tafadhali Yahwe, uiokoe nafsi yangu.”
5Yahwe ni mwenye neema na haki; Mungu wetu ni mwenye huruma.
6Yahwe huwalinda wasio na hila; nilishushwa chini akaniokoa.
7Nafsi yangu inaweza kurudi mahali pake pa kupumzika, kwa kuwa Yahwe amekuwa mwema kwangu.
8Kwa maana uliokoa uhai wangu dhidi ya kifo, mcho yangu dhidi ya machozi, na miguu yangu dhidi ya kujikwaa.
9Nitamtumikia Yahwe katika nchi ya walio hai.
10Nilimwamini yeye, hata niliposema, “nimeteswa sana.”
11Kwa haraka nilisema, “Watu wote ni waongo.”
12Nimlipeje Yahwe kwa wema wake wote kwangu?
13Nitakiinua kikombe cha wokovu, na kuliitia jina la Yahwe.
14Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote.
15Mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pa Mungu.
16Ee Yahwe, hakika, mimi ni mtumishi wako; mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umefungua vifungo vyangu.
17Nitakutolea dhabihu ya shukrani na nitaliitia jina la Yahwe.
18Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote,

19katika nyua za nyumba ya Yahwe, katikati yako, Yerusalemu. Msifuni Yahwe.