Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 101

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nitaimba uaminifu wa agano lako na hukumu; kwako, Ee Yahwe, Nitakuimbia sifa.
2Nitatembea katika njia ya uadilifu. Oh, ni lini utakuja kwangu? Nitatembea kwa uadilifu ndani ya nyumba yangu.
3Sitaweka matendo maovu mbele ya macho yangu; ninachukia uovu usio na maana; hauta shikamana nami.
4Watu waliopotoka wataniacha mimi; mimi sichangamani na uovu.
5Nitamwangamiza yeyote amsengenyaye jirani yake kwa siri. Sitamvumilia yeyote mwenye kiburi.
6Nitawachagua walio waaminifu katika nchi wakae upande wangu. Wale watembeao katika njia ya uhadilifu watanitumikia.
7Watu wadanganyifu hawatabaki ndani ya nyumba yangu; waongo hawatakaribishwa mbele ya macho yangu.
8Asubuhi hata asubuhi nitawaangamiza waovu wote kutoka nchini; nitawaondoa watendao maovu wote katika mji wa Yahwe.