Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde
2na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni.
3Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa.
4Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.
5Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki.
6Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye.
7Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu.
8Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima!
9Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.