Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 103

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, na vyote vilivyomo ndani yangu, nitalisifu jina lake takatifu.
2Maishani mwangu mwote nitamsifu Yahwe, na kukumbuka matendo yake yote mazuri.
3Yeye husamehe dhambi zako zote; huponya magonjwa yako yote.
4Huukomboa uhai wako dhidi ya uharubifu; hukuvika taji kwa uaminifu wa agano lake na hutenda kwa rehema.
5Huyatosheleza maisha yako kwa mambo mema ili kwamba ujana wako ufanywe upya kama tai.
6Yahwe hutenda yaliyo haki naye hutenda hukumu ya haki kwa ajili ya wote walio onewa.
7Alimjulisha Musa njia zake, matendo yake kwa uzao wa Israeli.
8Yahwe ni wa huruma na neema; ni mvumilivu; ana agano kuu la uaminifu.
9Hataadhibu siku zote; hakasiriki siku zote.
10Hatushughulikii sisi kama dhambi zetu zinavyostahili au kutulipa kulingana na uhitaji wa dhambi zetu.
11Kama mbingu zilivyo juu zaidi ya nchi, ndivyo ulivyo ukuu wa uaminifu wa agano lake kwao wale wanaomcha yeye.
12Kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi, hivi ndivyo ameondoa hatia zetu za dhambi zetu mbali nasi.
13Kama vile baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Yahwe alivyo na huruma kwao wamchao.
14Maana anajua tulivyo umbwa; anajua kuwa tu mavumbi.
15Kama ilivyo kwa mwanadamu, siku zake ni kama majani; hustawi kama ua katika shamba.
16Upepo hulipiga, nalo hutoweka, na hakuna hata mmoja awezaye kuelezea mahali lilipokua.
17Lakini agano la uaminifu wa Yahwe uko kwa wale wamchao yeye milele hata milele. Haki yake ni endelevu kwa uzao wao.
18Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maagizo yake.

19Yahwe ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake watawala juu ya kila mtu.
20Msifuni Yahwe, enyi malaika zake, ninyi hodari wenye nguvu na mtendao neno lake, na kutii sauti ya neno lake.
21Msifuni Yahwe, enyi jeshi la malaika wote, ninyi ni watumishi mfanyao mapenzi yake.
22Msifuni Yahwe, viumbe wake wote, mahali popote atawalapo. Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote.