1“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme.
2“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda.
3Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu.
4Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.”
5Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni.
6Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua,
7ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.
8Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”