Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 126

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.
2Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.”
3Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo!
4Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini.
5Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.
6Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.