Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 112

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake.
2Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa.
3Nyumbani mwake mna utajiri na mali; na haki yake itadumu milele.
4Nuru huangazia gizani kwa ajili ya mtu mcha Mungu; yeye ni wa fadhili, huruma, na haki.
5Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu.
6Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele.
7Haogopi habari mbaya; ni jasiri, akimtumainia Yahwe.
8Moyo wake ni mtulivu, hana woga, mpaka aonapo ushindi dhidi ya watesi wake.
9Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima.
10Mtu mwovu ataona haya na kukasirika; atasaga meno yake na kuyeyuka; tamaa ya wasio haki itapotea.