1Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano.
2Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio.
3Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele.
4Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema.
5Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake.
6Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika.
8Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri.
9Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha.
10Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.