Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 102

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sikia maombi yangu, Ee Yahwe; sikia kulia kwangu kwako.
2Usiufiche uso wako mbali nami wakati wa shida. Unisikilize. Nikuitapo, unijibu upesi.
3Kwa maana siku zangu zinapita kama moshi, na mifupa yangu kama moto.
4Moyo wangu umeumizwa na niko kama majani yaliyo kauka. Ninasahau kula chakula chochote.
5Kwa muendelezo wa kuugua kwangu, nimekonda sana.
6Niko kama mwali wa jangwani; nimekuwa kama bundi magofuni.
7Ninalala macho kama shomoro faraghani, pekeyake juu ya paa.
8Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; wale wanao nidhihaki hutumia jina langu katika laana.
9Ninakula majivu kama mkate na kuchanganya kinywaji changu kwa machozi.
10Kwa sababu ya hasira yako kali, umeniinua juu kunitupa chini.
11Siku zangu ni kama kivuli kanachofifia, na ninanyauka kama majani.
12Lakini wewe, Yahwe, unaishi milele, na kumbukumbu lako ni kwa vizazi vyote.
13Wewe utasimama na kuirehemu Sayuni. Sasa ni wakati wa mkurehemu yeye. Wakati ulio teuliwa umefika.
14Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake pendwa na kuyaonea huruma mavumbi ya magofu yake.
15Mataifa wataliheshimu jina lako, Yahwe, na wafalme wote wa nchi watauheshimu utukufu wako.
16Yahwe ataijenga tena Sayuni na ataonekana katika utukufu wake.
17Wakati huo, atajibu maombi ya fukara; hatayakataa maombi yao.
18Hii itaandikwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na watu ambao bado hawajazaliwa watamsifu Yahwe.

19Maana ametazama chini toka mahali pa juu patakatifu;
20Toka mbinguni Yahwe ameiangalia nchi, ili kusikia kuugua kwa wafungwa, kuwafungua waliohukumiwa kufa.
21Kisha watu watalitangaza jina la Yahwe katika Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu
22pindi mataifa na falme watakapokusanyika pamoja kumtumikia Yahwe.
23Amechukua nguvu zangu katikati ya siku zangu za kuishi, amezifupisha siku zangu.
24Nilisema, “Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; wewe uko hapa hata kizazi chote.
25Tangu zama za kale wewe uliiweka nchi mahali pake; mbingu ni kazi ya mikono yako.
26Mbingu na nchi zitaangamia lakini wewe utabaki; zitachakaa kama mavazi; utaziondoa kama watu waondoavyo mavazi yaliyo chakaa, nazo hazitaonekana tena.
27Lakini wewe ni yuleyule, na miaka yako haitakuwa na mwisho.
28Watoto wa watumishi wako wataendelea kuishi, na uzao wao utaishi katika uwepo wako.