1Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni,
2Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli.
3Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma.
4Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo.
5Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma?
6Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo?
7Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo.
8Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.