Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 47

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi.
2Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote.
3Yeye anawatiisha chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu.
4Yeye huchagua urithi kwa ajili yetu, utukufu wa Yakobo ambaye alimpenda. Serah
5Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu.
6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa.
8Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi.
9Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Ibrahimu; kwa kuwa ngao za duniani ni za Mungu; yeye ameinuliwa juu sana.