Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote, wewe ufunuaye utukufu wako juu mbinguni.
2Kutoka katika midomo ya watoto na vichanga umeumba sifa kwa sababu ya utukufu wako, ili kuwanyamazisha maadui wote na walipa kisasi wote.
3Ninapozitazama mbingu, ambazo vidole vyako vimeumba, mwezi na nyota, ambazo umeziweka kila mmoja katika nafasi yake,
4Binadamu ni nani hata umtazame, na watu hata uwajali wao?
5Umewaumba chini kidogo kuliko viumbe vya mbinguni na umewazunguka na utukufu na heshima.
6Umemfanya binadamu kutawala kazi ya mikono yako; umeviweka vitu vyote chini ya miguu yake:
7kondoo na ng'ombe wote, na hata wanyama wa porini,
8ndege wa angani, na samaki wa baharini, na vyote vipitavyo katika mikondo ya bahari.
9Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote!