Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 128

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake.
2Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa.
3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako.
4Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa.
5Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.
6Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.