Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 87

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;
2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.
3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah
4Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”
5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.
6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah
7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”