Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa nini, Yahweh, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?
2Kwa sababu ya majivuno yao, watu waovu waawakimbiza wanyonge; Basi tafadhari uwafanye waovu kunaswa kwa mipango yao wenyewe walioipanga.
3Kwa kuwa mtu mwovu hujivuna kwa tamaa yake ya ndani; yeye hufurahisha tamaa na kumtusi Yahweh.
4Mtu mwovu ameinua uso wake; naye hamtafuti Mungu. Yeye hamfikilii Mungu kamwe kwa kuwa hamjali kabisa Mungu.
5Yeye yuko salama wakati wote, amri zako za haki ziko juu sana kwake; naye huwadharau adui zake wote.
6Yeye husema moyoni mwake, “Siwezi kamwe kushindwa; katika kizazi chote sitakutana na shida.”
7Mdomoni mwake kumejaa kulaani na udanganyifu, maneno yenye sumu; ulimi wake unajeruhi na kuharibu.
8Yeye husubilia kwenye shambulio karibu na kijiji; mahali pa siri huwauwa watu wasio na hatia; macho yake huwatazama wasionahatia.
9Hujibanza mahari pa siri kama simba katika kichaka; yeye hulala akisubiri kumkamata mnyonge. Humkamata pale anapokwisha mweka mtegoni mwake.
10Wanyonge wake hugandamizwa chini na kupigwa; wao huangukia katika mtego imara.
11Yeye husema katika moyo wake, “Mungu amesahau; huficha uso wake; hawezi kujishughulisha kutazama.”
12Inuka, Yahweh! Inua mkono wako, Mungu! Usiwasahau wanyonge.
13Kwa nini mtu mwovu anamkataa Mungu na kusema moyoni mwake, “Hautanipata katika hatia?”
14Umeona, maana mara zote unaangalia mtu aletaye madhara na jeuri. Mtu asiye na msaada hukuachia nafsi yake; maana wewe huwaokoa yatima.
15vunja mkono wa mwovu lo na mtu mwovu. Umuajibishe kwa matendo yake maovu, ambayo kwayo alifikiri hautayagundua.
16Yahweh ni mfalme milele daima; mataifa yanaondolewa katika aridhi yake.
17Yahweh, umesikia uhitaji wa wanyonge; nawe umeitia nguvu mioyo yao, wewe unasikia maombi;
18Unawatetea yatima na wanyonge ili kusudi pasiwepo na mtu katika dunia hii atakaye leta hofu tena.