1Ni kwako Yahweh ninapata usalama; ni kwa namna gani utasema na mimi, “Ruka kama ndege hadi mlimani”?
2Tazama! Waovu wana andaa pinde zao. Wana tayarisha gizani mishale yao kwenye kamba ili kufyatua mioyo ya wenye haki.
3Ikiwa misingi imeharibiwa, mwenye haki atafanya nini?
4Yahweh yuko katika hekalu takatifu; macho yake yanatazama, yakiuchunguza ubinadamu.
5Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine.
6Yeye huwanyeshea waovu makaa ya mawe na moto wa jehanamu; upepo uunguzao utakuwa ni sehemu yao kutoka katika kikombe chake!
7Kwa kuwa Yahweh ni mwenye haki, Naye hupenda haki; wenye haki watauona uso wake.