Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 73

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale walio na moyo safi.
2Lakini kwangu mimi, kidogo tu miguu yangu iteleze; miguu yangu karibu iteleze kutoka kwangu
3kwa sababu niliwaonea wivu wenye kiburi nilipoona mafanikio ya waovu.
4Kwa maana hawana maumivu hadi kufa kwao, lakini wana nguvu na wameshiba.
5Wako huru dhidi ya mizigo ya watu wengine; nao hawateswi kama watu wengine.
6Kiburi kinawapamba kama mkufu kwenye shingo zao; jeuri huwavika kama vazi.
7Katika upofu wa jinsi hii dhambi huja; mawazo maovu hupita mioyoni mwao.
8Wao hudhihaki na kuongea kwa namna ya uovu; kwa kiburi chao hutishia mateso.
9Wameweka vinywa vyao dhidi ya mbingu, na ndimi zao hutanga tanga duniani.
10Kwa hiyo watu wake huwageukia na maji yaliyojaa hukaushwa.
11Nao husema, “Mungu anajuaje? Yako maarifa kwake yeye aliye juu?”
12Fahamu: watu hawa ni waovu; mara zote hawajali, wakifanyika matajiri na matajiri.
13Hakika nimeutunza moyo wangu bure na nimenawa mikono yangu pasipo kukosa.
14Maana mchana kutwa nimeteswa na kuadhibiwa kila asubuhi.
15Kama ningesema, “Ningesema mambo haya,” kumbe nigewasaliti kizazi hiki cha watoto wenu.
16Ingawa nilijaribu kuyaelewa mambo haya, yalikuwa ni magumu sana kwangu.
17Ndipo nilipoingia patakatifu pa Mungu na kuelewa hatma yao.
18Hakika wewe huwaweka penye utelezi; huwaangusha mpaka palipoharibika.

19Jinsi gani wamekuwa ukiwa kwa muda mfupi! Wamefika mwisho nao wamemaliza kwa utisho.
20Wao ni kama ndoto wakati wa mtu kuamka; Bwana, utakapo inuka, utazidharau ndoto zao.
21Maana moyo wangu ulipata uchungu, nami nilijeruhiwa sana.
22Nilikuwa mjinga na sijui neno; nilikuwa kama mnyama tu mbele yako.
23Lakini mimi nipo pamoja nawe daima; umenishika mkono wa kuume.
24Utaniongoza kwa shauri lako na baadaye utanipokea katika utukufu.
25Ni nani niliye naye mbinguni isipokuwa wewe? Hakuna nimtamaniye duniani isipokuwa wewe.
26Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.
27Wale walio mbali nawe wataangamia; utawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
28Lakini mimi, linipasalo kufanya ni kumkaribia Mungu. Nimemfanya Bwana Yahwe kimbilio langu. Nami nitayatangaza matendo yako yote.