Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 109

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Zaburi ya Daudi. Mungu ninaye msifu, usinyamaze kimya.
2Kwa maana waovu na wadanganyifu wananishambulia; wanazungumza uongo dhidi yangu.
3Wananizunguka na kusema mambo ya chuki, na wananishambulia bila sababu.
4Wananilipa kashfa badala ya upendo, lakini mimi ninawaombea.
5Wananilipa uovu badala ya mema, na wanachukia upendo wangu.
6Teua mtu mwovu aliye adui zaidi kama watu hawa; teua mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7Na atakapohukumiwa, aonekane na hatia; maombi yake yachukuliwe kuwa ni dhambi.
8Siku zake na ziwe chahe; mamlaka yake na yachukuliwe na mtu mwingine.
9Watoto wake wawe yatima, na mke wake awe mjane.
10Watoto wake wenye kutanga tanga na kuombaomba, wakiondoka katika nyumba zao zilizo haribika na kuomba chakula au pesa kwa wapita njia.
11Mdai na achukue vitu vyake vyote amilikivyo; wageni wateke mapato ya kazi yake.
12Asiwepo mtu yeyote wa kumfanyia wema; mtu yeyote asiwahurumie yatima wake.
13Watoto wake waangamizwe; majina yao na yafutwe katika kizazi kijacho.
14Uovu wa baba zake utajwe kwa Yahwe; na dhambi ya mama yake isisahaulike.
15Hatia zao na ziwe mbele ya Yahwe siku zote; Yahwe na aiondoe kumbukumbu yao duniani.
16Yahwe na afanye hivi kwa sababu mtu huyu kamwe hakusumbuka kuonesha uaminifu wa agano wowote, lakini badala yake aliwasumbua wanyonge, wahitaji, na kuwaua walio vunjika moyo.
17Alipenda kulaani; na imrudie juu yake. Alichukia kubariki; baraka zozote na zisije kwake.
18Alijivika kulaani kana kwamba ni vazi lake, na laana yake iliingia ndani yake kama maji, na kama mafuta mifupani mwake.

19Laana zake na ziwe kwake kama vazi avaalo kujifunika mwenyewe, na kama mkanda avaao kila siku.
20Na haya yawe malipo ya mshitaki wangu kutoka kwa Yahwe, ya wale wasemao mambo maovu juu yangu.
21Yahwe Bwana wangu, unishughulikie kwa wema kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni mwema, uniokoe.
22Kwa maana ni mnyonge na muhitaji, na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23Ninatoweka kama kivuli cha jioni; ninapeperushwa kama nzige.
24Magoti yangu ni dhaifu kutokana na kufunga; ninakuwa mwembamba na mifupa.
25Nimedharauliwa na washitaki wangu; wanionapo; hutikisa vichwa vyao.
26Nisaidie, Yahwe Mungu wangu; uniokoe kwa uaminifu wa agano lako.
27Nao wajue kuwa wewe umefanya haya, kwamba wewe, Yahwe, umetenda haya.
28Ingawa wananilaani, tafadhali unibariki; wanishambuliapo, waaibishwe, lakini mtumishi wako afurahi.
29Washitaki wangu na wavishwe kwa aibu; wavae aibu yao kama vazi.
30Kwa kinywa changu ninatoa shukrani kuu kwa Yahwe; nitamsifu yeye katikati ya kusanyiko.
31Maana nitasimama mkono wa kuume wa mhitaji, ili nimuokoe dhidi ya wale wanao muhukumu.