1“Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa,
2“Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu,
3basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu.
4Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia.
5Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.”
6Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao.
7Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka.
8Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.